Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Honour Janza amekitaja kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, kitakachoingia kambini kwaajili ya michezo miwili ya kirafiki na Libya kwenye kalenda ya FIFA.

Kikosi cha Taifa Stars Dhidi ya Libya Chatajwa.

Majina mapya ya wachezaji waliongezeka kwenye kikosi hicho tofauti na kile kilichocheza na timu ya taifa ya Uganda, ni takribani 15, yakiwa na wachezaji kutoka Ligi tofauti kama vile Said Hamis anayechezea Hatta Club ya Falme za Kiarabu, David Uromi anayekipiga Moroka Swallows ya Afrika KUSINI.

Kubwa zaidi kwenye kikosi hicho ni kukosekana kwa majina ya wachezaji waliozoeleka kwenye Timu ya Taifa, wachezaji hao ni Bakari Nondo Mwamnyeto, Mohammed Hussein, Kibu Denis, Jonas Mkude, Salum Abubakar. pamoja na John Raphael Bocco.

Kikosi cha Taifa Stars Dhidi ya Libya Chatajwa.

Taifa Stars watacheza mechi hizo mbili za kirafiki ambazo zipo kwenye kalenda ya FIFA, na timu ya Taifa ya Libya, licha ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha kwa Watanzania watapaswa kushinda mechi hizi mbili za kirafiki ili kujiongezea alama za viwango kimataifa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa