Real Madrid wametangaza kupata faida ya paundi Milioni 11 sawa na Euro (€13m) katika mwaka wa fedha uliopita licha ya athari za kifedha za Uviko-19 kwenye LaLiga.

Habari hizi zinakuja baada ya rais wa klabu hiyo Florentino Perez kufanya mkutano na wanahisa wa klabu ili kuwapa taarifa kuhusu hali ya kifedha Santiago Bernabeu.

Real Madrid Wapata Faida £11M

Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya mabingwa hao wa Uhispania ilisema kuwa thamani ya klabu hiyo ilifikia paundi milioni 473 sawa na Euro (€546m) mwezi Juni – ongezeko kwa msimu wa tatu mfululizo na kupanda kutoka paundi milioni 463 za mwaka jana sawa na Euro (€534m).

Klabu hiyo pia ilitangaza kuwa paundi milioni 368 (€425m) zipo kwaajili ya matumizi ya klabu hiyo vile watakavyo.

Real Madrid Wapata Faida £11M

Taarifa hiyo inaongeza mapato ya uendeshaji wa Madrid mwaka 2021-22 yaliongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka uliopita wa fedha, na kupanda kutoka Paundi Milioni 566 (€653M) hadi £626M sawa na (€722M).

Mavuno hayo yanakuja licha ya ukweli kwamba mabingwa hao mara 14 wa Uropa walipoteza takribani paundi Milioni 347 (€400m) kutokana na janga hilo.

Real Madrid Wapata Faida £11M

Madrid pia ilirudisha paundi Milioni 8 (€10m) zaidi katika mauzo ya wachezaji kuliko walivyotumia kuongeza wachezaji wapya kwenye soko la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Real Madrid Wapata Faida £11M
Cristiano Ronaldo akishangilio moja ya bao kwa mtindo wake maarufu wa ‘Siuuu’ uwanja wa Bernabéu. (2017/18)

Matokeo hayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na mauzo ya Paundi (£70m) ya kiungo wa kati wa Brazil Casemiro kwenda Manchester United, ada ya tatu kwa ukubwa zaidi kuwahi kukusanywa, nyuma ya Angel Di Maria na Cristiano Ronaldo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa