Rais wa Young Africans SC Eng.Hersi Said amesema wapo kwenye moja ya Kundi gumu la Ligi ya Mabingwa Afrika lakini watajitahidi waweze kuwa miongoni mwa timu mbili za juu ili kufuzu Robo Fainali ya CAF.
Kuhusu Al Ahly, Eng. Hersi Said amedai kuwa ni kipimo kizuri kwao kama Yanga kucheza na Bingwa mtetezi na hilo litawaonesha kwa kiasi gani mpira wao umekuwa.
”Ni kipimo kizuri kwetu kupata nafasi ya kucheza na Al Ahly Bingwa mtetezi, ni kipimo kizuri pia kwetu kuona jinsi gani tumekuwa (Kisoka) kama Klabu ya Mpira”
“Naona ni moja katika makundi magumu lakini Young Africans tunatakiwa sasa tuweke jitihada kuwa katika timu mbili za juu zitakazokwenda kwenye Robo Fainali.”

