GAMONDI MATUMAINI KIBAO MBELE YA MAMELODI

KOCHA wa Yanga Miguel Gamondi amesema kuwa kutokana na kile ambacho amekiandaa kwenye Uwanja wa mazoezi Kuna uwezekano mkubwa wa timu yake kufanya vema dhidi ya Mamelodi Sundowns leo.

Yanga watashuka Uwanjani saa 3 usiku leo, kucheza na Mamelodi ukiwa ni Mchezo Wa marudiano utakaoamua kama Wanakwenda nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika au wanarudi Nyumbani.gamondiKwenye, maandalizi yake ya mwisho jana Gamondi aliwatumia wachezaji wake wote waliosafiri kwenda Afrika Kusini.

“Nina Imani Kuna kitu kizuri kitafanyika uwanjani, wachezaji wangu wameonekana kuwa na ari na morali kuelekea kwenye mchezo huo. Siyo mchezo rahisi kwetu.gamondi“Lakini Kuna Kila Sababu ya sisi kufanya vema Kwa kuwa Kila mmoja anajua umuhimu wa kufanya vizuri ndani ya dakika tisini,” alisema Gamondi.

Acha ujumbe