Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Ange Postecoglou amesema mshambualiaji wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Brazil Richarlison atakosekana katika mchezo wa jumapili dhidi ya klabu ya Nottingham Forest.
Mshambuliaji Richarlison kukosekana kwake katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Nottingham Forest kutokana na majeraha aliyoyapata katika goti lake, Lakini kuna uwezekano akapatikana katika mchezo dhidi ya Newcastle United.Kocha wa Ange amethibitisha taarifa hiyo akiongea na waandishi wa habari leo mshambuliaji huyo siku za hivi karibuni amekua akifanya vizuri ndani ya klabu hiyo, Kuanza kuandamwa na majeraha sio jambo zuri kwa ustawi wa kiwnago chake.
Klabu ya Tottenham hivi karibuni imekua ikikumbana na majeraha kwenye kikosi chake jambo ambalo limefanya klabu hiyo kusuasua hivi karibuni, Jambo linatia wasiwasi kwa klabu hiyo kuelekea kuipata nafasi ya kufuzu ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.Mshambuliaji Richarlison yeye ana asilimia kubwa za kurejea kwenye mchezo dhidi ya Newcastle United baada ya kuukosa mchezo dhidi ya Nottingham Forest, Msimu huu ulionekana kuanza kukaa vizuri kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil japokua amekua akiandamwa na majeraha ya hapa na pale.