BAADA ya kuachana na wachezaji wao tisa, Uongozi wa Kagera Sugar umefunguka kuwa hawaathiriki na uamuzi huo kwani tayari wamepata wachezaji watakaochukua nafasi hizo kwenye kikosi.
Mara baada ya kumalizika kwa msimu huu tayari Kagera Sugar wamewaacha wachezaji tisa wakiwemo Hassan Mwaterema na Nassoro Kapama aliyetambulishwa na Simba hivi karibuni.
Kagera, Kagera Sugar Wapata Mbadala wa Kapama, Meridianbet
Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Kagera Sugar, Hamis Mzanzala amesema kuwa “Mipango yetu kwa msimu uliopita yalikuwa ni kumaliza ligi kwenye nafasi nne za juu katika msimamo lakini haikuwa hivyo ila msimu ujao tunaenda kuanza tulipoishia.
“Tayari tumeachana na wachezaji tisa lakini hiyo haituathiri kwani tumepata wachezaji ambao wataenda kuchukua hizo nafasi kwa ajili ya kutimiza malengo ya klabu kwa msimu ujao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa