KIUNGO mwenye vituko vingi nje ya uwanja Bernad Morrison amefunguka kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa na Yanga na kubwa zaidi akiwataka wanayanga wampokee kwa kuwa amerudi nyumbani.

Bernad ‘BM3gh’ aliweka ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akielezea hisia zake baada ya kurejea kwenye timu hiyo, akisema anajua aliwakosea wanayanga na amerudi kuja kufanya kazi na kuwafurahisha Wananchi.

Morrison, Morrison: Yanga Nipokeeni Mtoto Wenu Nimerudi Nyumbani, Meridianbet

Morrison aliandika: “Nilikuwa hapa, nikaondoka sasa nimerudi tena, naamini ujio huu wa pili utakuwa mkubwa kuliko ule wa mara ya kwanza, Nilipendwa na Taifa hili la rangi ya njano na kijani na bado mnanipenda.

“Najua niliwasababishia maumivu na aibu bado mmenipokea mtoto wenu wenu nirudi nyumbani kwasababu sote tunajua nyumbani kutamu.

“Kijana wenu nimerudi na nitafanya niwezavyo kuwafanya muwe na furaha kila mahali na wakati wote. Tushirikiane kuiweka klabu hii ya Mabingwa kwenye jukwaa la kimataifa kama ilivyokuwa ikifanya hapo awali.”

Morrison amerejea tena Yanga baada ya kumaliza mkataba wake wa kuitumikia Simba, alipodumu kwa misimu miwili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa