BAADA ya Metacha Mnata kutambulishwa na Singida Big Stars, Uongozi wa Polisi Tanzania umefunguka kuwa kipa huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo.
Metacha alitambulishwa na klabu ya Singida Big Stars hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Polisi Tanzania.
polisi
Akizungumzia jambo hilo, Katibu Mkuu wa Polisi Tanzania, Michael Mtebene amesema kuwa “Tumeshangaa kutambulishwa kwa Metacha na klabu ya Singida Big Stars.
“Metacha bado ni mchezaji wetu na tuna mkataba naye wa mwaka mmoja kwani wakati anasaini kwetu msimu uliopita alisaini miaka miwili hivyo taratibu mbalimbali tutazifuata.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa