Sadio Kanoute kiungo wa kimataifa wa Mali imethibitishwa na uongozi wa klabu ya Simba SC kuwa ameshindwa kusafiri na timu hiyo na atakosa michezo yao miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Asante Kotoko na Al Hiilal nchini Sudan baada ya kuruhusiwa kwenda kwao kwa ajili ya kushughulikia pasi yake ya kusafiria.

Kutokana na changamoto ya pasi hiyo ya kusafiria Kanoute alichelewa kambi ya wiki nne ambayo timu hiyo waliiweka mwanzoni mwa msimu huu nchini Misri.

Kanoute: Kiungo wa Mali Ashtua Simba SC
Kiungo wa Simba SC Sadio Kanoute

Kikosi cha Simba SC kiliondoka nchini alfajiri ya kuamkia Alhamis na wachezaji 19 kuelekea nchini Sudani kwa ajili ya mashindano mafupi ‘Mini Tournament’ ambapo wanatarajia kuwa na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Asante Kotoko na Al Hilal.

Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally alisema: “Ni kweli kiungo wetu mkabaji Sadio Kanoute hayupo kwenye sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kimesafiri kuelekea Sudani kwa ajili ya mashindano madogo ‘Mini Tournament’ tuliyoalikwa na timu ya Al Hilal.

Kanoute: Kiungo wa Mali Ashtua Simba SC
Ahmed Ally- Meneja habari na mawasiliano Simba SC

“Hii ni kutokana na mchezaji huyo kuwa na dharula ya kurejea kwao Mali kushughulikia pasi yake ya kusafiria ‘VISA’ ambayo inakaribia kujaa na kumekuwa na changamoto kubwa ya kupata VISA mpya kutokana na hali ya kisiasa kwao.

“Hivyo uongozi uliona umpe nafasi ya kwenda kukamilisha hilo mapema kabla ya kuanza kwa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo yataanza mwezi Septemba.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa