Kisa Waarabu Yanga Yashtukia Mchongo

Mabingwa wa muda wote Tanzania na wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Yanga SC, Jana Novemba 04, 2022 walikwea mwewe kuwafuata waarabu wa Tunisia, Club Africain, kwenye mchezo wa marudio.

Yanga SC walilazimika kupitia Dubai na kupumzika kwa siku moja kabla ya kuanza safari ya kwenda Tunisia hii leo, kitu ambacho kinawapa nafasi ya kupumzika na kukwepa hujuma za Waarabu.

 

Kisa Waarabu Yanga Yashtukia Mchongo

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Novemba 9 mwaka huu ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar Es Salaam, ulimalizika kwa sare ya kutokufungana.

Hivyo ili Yanga waweze kuvuka katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Shirikisho wanapaswa kushinda au kutoa sare ya magoli yeyote, ila mchezo kama utamalizika kwa sare ya kutokufungana itabidi mikwaju ya penati iamue nani anakuwa mshindi.

Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema “Tumeumizwa na matokeo yaliyopita ya suluhu na hakuna mtu yeyote ambaye amejiandaa nayo. Tunawaomba wana Yanga kuwa wamoja na kuisapoti timu yetu tunaamini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye dakika 90 za mchezo wa marudiano kule Tunisia.

 

Kisa Waarabu Yanga Yashtukia Mchongo

“Kwenye mpira lolote linawezekana tumefanya vibaya kwenye mchezo wa nyumbani kwa kutoka suluhu lakini tutaenda kupambana kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano.”

Yanga SC walianzia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika na kutolewa, na AL-HILAL ya nchini Sudan.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

Bonyeza hapa

Acha ujumbe