Kiungo Simba Nje Wiki Mbili

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Peter Banda atakuwa nje ya kikosi hicho kwa wiki mbili kwa ajili ya kuuguza jeraha lake la mguu.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kikosi chao kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Namungo.

“Timu iko vizuri na inaendelea na mazoezi kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Namungo.

“Tunatambua utakuwa mchezo mgumu sana kwani mara zote ambazo tunakutana licha ya kwamba tunashinda lakini tunapata ushindani mkubwa sana kutoka kwao.

“Mchezaji mwenye majeraha mpaka sasa ni Peter Banda ambaye anasumbuliwa na majeraha ya mguu hivyo dokta amesema atakuwa nje kwa wiki mbili akiuguza jeraha.”

Acha ujumbe