Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula anazipigia mahesabu pointi tatu za mchezo wao wa pili kwenye ligi ya mabingwa Afrika kwa wanawake dhidi ya Determine Girls ya Liberia.
Mpaka sasa Simba Queens hawajaambulia pointi yeyote kwenye ligi hiyo hiyo ni baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya AS Far Rabat ya Morocco.

Akizungumzia maandalizi yao, Lukula alisema: “Tunataka kwenye hiyo mechi ijayo tupate ushindi na sio mabao mengi.
“Tukipata pointi tatu hizo zitatufanya kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Green Buffalo tupate ushindi ili tumalize katika nafasi ya pili na tuvuke hatua inayofuata.
“Nina imani kubwa na wachezaji wangu wataenda kupambana zaidi ili kutimiza malengo ya timu pamoja na malengo yao binafsi kwenye haya mashindano.”

