Mshambuliaji wa Young Africans SC Fiston Mayele ambaye pia ni Raia wa DR Congo amemfananisha kiungo wa Yanga Feisal Salum “Fei Toto” kama Thiago Alcantara ambaye ni kiungo wa Liverpool.

Mayele ambaye jana alikuwa na mchezo mzuri, aliweza kufanga hat-trick yake ya kwanza kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa, akiweka rekodi baada ya kupita miaka nane bila mchezaji yeyote wa Ligi ya Tanzania kufunga hat-trick, mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2014 Mrisho Ngasa alifunga Hat-trick kwenye hatua ya awali.
Katika ukurasa wake wa Twitter Mayele aliposti picha akiwa yeye na Feisal huku akisindikiza na maandishi “Thiago Alcantara” akimaanisha kwamba Fei ni kama Kiungo wa Liverpool Alcantara.
Yanga SC ilianza vizuri kwenye mechi yake ya kwanza kwa kuwachalaza vibaya Zalan FC ya Nchini Sudan Kusini mabao 4-0 huku Fiston akizama nyavuni mara tatu na Feisal akizama mara moja.
View this post on Instagram
Mechi ya pili itampaswa Yanga asifungwe goli zaidi ya 4, ili aweze kuendelea kwenye hatua ya Kwanza ambapo kama atafanikiwa kufuzu atakutana na mshindi katika ya AL Hilal ya Sudan au St George FC kutoka Ethiopia.