Klabu ya RS Berkane ya nchini Morroco inayoshiriki ligi maarufu ijulikanayo kama Botola  imebeba kombe lao la kwanza la CAF Super Cup hapo jana baada ya kuitungua Wydad Casablanca kwa mabao 2-0.

 

 Berkane Mabingwa wa SuperCup 2022

 

RS Berkane ambao ndio mabingwa wa michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika walichukua taji hilo mbele ya mabingwa wa klabu bingwa barani Afrika Wydad Casablanca ambao wao walichua kombe hilo la klabu bingwa kutoka kwa Al Ahly.

Berkane wamekuwa na ubora sana kiasi kwamba sio rahisi inapofika suala la michezo ya fainali inatakiwa timu ijipange haswa kwani wamekuwa na kiwango kizuri sana katika mechi hizi za mashindano makubwa barani Afrika.

 

 Berkane Mabingwa wa SuperCup 2022

Klabu hiyo imechukua makombe mbalimbali ikiwemo kombe la ligi walilochukua mwaka 2012, wakafuzu kucheza michuano ya kombe la shirikisho mwaka 2019, huku mwaka 2020 wakibeba kombe la shirikisho barani Afrika na baada ya miaka miwili wakalichukua tena  na hapo jana wakabeba kombe la CAF Super Cup ambapo hukutana mabingwa wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Mabingwa wa Shirikisho Afrika, ambapo walifanikiwa kushinda dhidi ya Wydad.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa