Kocha mkuu wa Atletico Madrid Diego Simeone amewasifia wachezaji wake kwa matokeo mazuri waliyoyapata wakiwa nyumbani baada ya kushinda mabao 4-1 dhidi ya Celta Vigo wakiwa nyumbani kwao huku ukiwa ni ushindi mnono kabisa.

 

Simeone Awasifu Wachezaji Wake

Mabao ya Angel Correa, Rodrigo De Paul, na Yannick Carrasco yaliongezwa kwa bao la kujifunga la Unai Nunez baada ya Gabriel Veiga kufungwa bao la kufutia machozi kwa Celta Vigo. Ilikuwa ni mara ya tatu kwa Atletico Madrid kufunga angalau mabao manne nyumbani kwenye Laliga msimu hu, moja tuu pungufu kuliko katika miaka minne iliyopita pamoja na kwenye mashindano mwaka 2018 moja, 2019 mawili, 2020 mara mbili.

Mchezo wao mwingine wa nyumbani walipoteza dhidi ya Villareal lakini wakafanya vizuri kwenye mchezo wao wa jana wakiwa nyumbani dhdi ya Celta Vigo.Akizungumza na DAZN baada ya ushindi huo Simeone alisema kuwa;

 

Simeone Awasifu Wachezaji Wake

“Baada ya kushindwa dhidi ya Villareal tulihitajika kuanza kuongeza alama kwenye Laliga, na kidogo kidogo tuliimarika”

Simeone alifanya mabadiliko tofauti na kile kikosi kilichocheza dhidi ya FC Porto ambapo walishinda kwa mabao mawili kwa moja, Anaendelea kusema kuwa. “Tulifanya mabadiliko mengi, tulijua kuwa baada ya Ligi ya Mabingwa mwili hauko sawa wala kichwa hakiwezi kuwa sawa’

Baada ya mchezo wao wa jana mchezo unofuata watacheza dhidi ya Bayer Leverkusen klabu bingwa halafu utafuata mchezo wa Dabi kati yao na Real Madrid ambapo watakuwa nyumbani.

 

Simeone Awasifu Wachezaji Wake

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa