Barcelona wametangaza kumkosa Ousmane Dembele wakiwa wanaenda kuumana na Celta Vigo.
Sergino Dest pia ameondolewa kwenye kikosi cha Jumamosi dhidi ya Celta Vigo kwenye gemu ya La Liga kwa sababu ya afya yake, Sergi Barjuan atakosa tena wachezaji muhimu.
Dembele na Dest wanaungana na Sergio Aguero, Martin Braithwaite, Pedri na Gerard Pique kuuguza majeraja, huku kukiwa na shaka juu ya Sergi Roberto.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuwa sawa na kile kilichoanza Jumanne na kushinda wa bao 1-0 dhidi ya Dynamo Kiev kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, jambo ambalo liliongeza matumaini ya Barcelona kutinga hatua ya 16 bora.
Luuk de Jong na Yusuf Demir pia ni chaguo la kwenye safu ya mashambulizi ya wana Catalan, ambayo bado iko chini ya usimamizi wa meneja wa muda Barjuan, wakati klabu ikiwa kwenye mchakato wa kufikia makubaliano na Al-Sadd juu ya Xavi.
Kikosi kinachotarajiwa cha Barcelona: Ter Stegen; Mingueza, R Araujo, Garcia, Alba; F de Jong, Busquets, Gavi; Coutinho, Memphis, Fati.
Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.


