Mshambuliaji hatari wa klabu ya Simba Moses Phiri amezua mijadala mbalimbali kwa kile kilichoonekana katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar na kumsababishia mchezaji huyo majeraha.
Mshambuliaji huyo ambaye aanaonekana kua hatari zaidi katika safu ya ushambuliaji ya Simba kwani akiwa amefunga mabao 10 mpaka sasa kwenye ligi kuu ya NBC, Amezua mijadala kwa wadau mbalimbali wa michezo kwa kudai mchezaji huyo anachezewa rafu mbaya na halindwi na waamuzi.
Katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao ulipigwa katika dimba la Kaitaba Kagera Sugar dhidi ya Mnyama Simba na kumalizika kwa suluhu ya goli moja kwa moja, Ni dhahiri mchezaji huyo alikua anachezewa radu mbaya mpaka kupelekea kupata majeraha lakini mwamuzi wa mchezo hakuchukua hatua yeyote kitu kilichofanya wadau mbalimbali wa soka kukemea kitendo hicho.
Mshambuliaji huyo kwasasa amepata majeraha ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa muda ambao haujajulikana bado, Mchezaji huyo ameonekana kuposti picha kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akiwa na magongo kuashiria amepata majeraha.
Taarifa ya kuumia kwa Moses Phiri imekua sio taarifa njema kwa mashabiki wa klabu ya Simba, Kwani mshambuliaji huyo ndio amekua akionekana msaada mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu ya Simba kwasasa.

