Mchezaji wa mkongwe wa klabu ya Liverpool James Milner pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Roberto Firmino wanajiandaa kukosekana katika mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Aston Villa.
Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema kua nyota wake wawili James Milner na mshambuliaji wake Roberto Firmino watakosekana katika mchezo kati wao kwanza wa mzunguko wa pili dhidi ya Aston Villa kutokna na majeraha.
Kocha huyo amesema James Milner atakosa michezo kadhaa huku Firmino yeye yupo kwenye hali nzuri na anaelekea kupona, Milner alitoka nje katika mchezo dhidi ya Manchester City siku ya jana ambapo walifungwa mabao matatu kwa mawili na kutupwa nje kwenye michuano ya Carabao Cup.
Kocha Jurgen Klopp pia amezungumzia kutokuwepo kwa beki wake wa kulia Trent Alexender Arnold ambaye hakufanya mazoezi na timu mpaka mwisho, Lakini kocha amesema anaamini atakua sawa kuelekea mchezo wao na Aston Villa.
Kocha Klopp amesema anafurahishwa kwakua wachezaji wote waliokua kwenye michuano ya kombe la dunia wamerejea kwenye timu, Lakini pia akisema wana kazi kubwa ya kuanza kufukuzia ubingwa kwani wanajua pengo la alama lililopo baina yao na viongozi wa ligi klabu ya Arsenal.

