BAADA ya kushinda mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Malindi, kesho jumatano kikosi cha Simba kinatarajia kushuka dimbani kumenyana tena na Kipanga FC kabla ya kurejea Dar.

 

Simba Kujipima na Kipanga Kesho

Kwenye mchezo huo uliopita Wekundu wa Msimbazi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 likifungwa na nyota wao mpya, Nassor Kapama.

 

Simba Kujipima na Kipanga Kesho

Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Juma Mgunda alisema kuwa “Kikosi kipo salama na maandalizi yanaendelea kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Kipanga

“Kesho tutakuwa tunacheza wawakilishi wawili kwenye michuano ya kimataifa na lengo la kucheza mechi hizi ni kupeana ujuzi zaidi kuelekea kwenye michuano ya kimataifa.

 

Simba Kujipima na Kipanga Kesho

“Ninawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kushuhudia mchezo huu na tutakuwa waungwana tukiwa uwanjani hivyo tunawaomba na wenzetu wawe waungwana ili mchezo uishe salama.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa