Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Juma Ramadhan Mgunda amesema kuwa kila mchezaji aliyesajiliwa na timu hiyo ni bora ana anayo nafasi ya kucheza na kila mmoja atapata muda wa kutoa mchango wake kwenye timu hiyo.

Mgunda alisema wapo wachezaji baadhi ambao wamekuwa hawapati muda wa kucheza kwa sasa, hiyo haimanishi kama uwezo wao mdogo, bali muda wao wa kucheza utafika na watacheza kadri watakavyotaka.

Mgunda, Mgunda: Simba Hii Atacheza Kila Mtu, Meridianbet

Mgunda alisema: “Hii ni timu kubwa yenye wachezaji wengi, kila mchezaji hapa ana nafasi kubwa ya kutoa mchango wake kwenye timu. Wote watacheza muda ukifika.

“Kila mchezaji aliyesajiliwa na Simba msimu huu na wale wote wanaounda timu yetu lazima watacheza. Lakini kila mmoja atacheza kwa muda wake.

“Haiwezekani wachezaji wote wacheze kwa wakati mmoja. Bali watacheza kwa kupeana nafasi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa