Andy Cole Amsifu Rashford Kurudi Kwenye Ubora.

Gwiji za zamani wa Manchester United Andy Cole, amemsifu mchezaji wa timu hiyo Marcus Rashford kwa kufanikiwa kurudi kwenye ubora wake msimu huu.

Mchezaji huyo ambaye alipitia kipindi kigumu msimu wa 2021/22 baada ya kuonesha kiwango duni sana katika msimu huo,Ambapo Rashford alifanikiwa kufunga mara tano katika michezo 32 ya mashindano yote huku klabu yake ikimaliza nafasi sita kwenye ligi kuu nchini humo.

andy coleMsimu huu mchezaji huyo tayari ana mabao matatu katika michezo sita baada ya kufunga bao moja dhidi ya Liverpool, na mabao mawili dhidi vinara wa ligi kuu nchini humo klabu ya Arsenal.

Licha ya kuboresha kiwango chake ila haikusaidia kumshawishi kocha wa timu ya taifa ya Uingereza kumrudisha kikosini katika mechi dhidi ya Ujerumani,pamoja Italy.

Andy Cole ambaye ameshinda mataji matano ya ligi kuu na klabu hiyo huku pia akishinda taji la ligi ya mabingwa ulaya ambalo ni maarufu zaidi baada ya kupindua meza dhidi ya Fc Bayern Munich mwaka 1998/99 anafurahishwa na kuona Rashford anarejesha makali yake msimu huu.

“Nafurahi kuona Rashford akifanya Vizuri,anafunga mabao itamrudishia kujiamini nafikiri analifurahia hilo”alisema Andy Cole

“Kama anaweza kumsukuma fowadi wa United msimu huu,sina hakika tutamaliza nafasi gani haswa,ila tukimaliza nafasi nne za juu itakua vizuri zaid”.

“Ni mara ya kwanza tunamuona Rashford anafanya mikimbio nyuma ya safu ya ulinzi ya timu pinzani tangu amepandishwa jwenye kikosi cha kwanza”.

andy cole“Nadhani alishuka msimu ulioisha, ambao ulikua wa kunyoosha timu” Ukiangalia anavyocheza sasa hivi, mpaka anaingia kwenye timu watu watageuka na kusema huyu ndo Marcus tunayemfahamu”

Andy Cole anaamini Rashford ataitwa kwenye kikosi cha Uingereza kitachoshiriki michuano ya kombe la dunia nchini Qatar kama ataendelea na kiwango hichi anachoonesha sasa.

Cole akijibu swali la mwandishi kuhusu uwezekano wa mchezaji kuitwa kwenye kikosi cha Uingereza “Nafikiri mtu pekee unaeweza kumuuliza kuhusu hilo ni Gary Southgate  mwenye timu yake”

“Siku zote sehemu ya kuonesha uwezo wako ni kwenye klabu, na kama ukifanya hivo utapata tu nafasi kwenye timu ya taifa”Alisema Andy Cole.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.