Simba Kushusha Mwingine Saa Tano Usiku

Klabu ya soka ya Simba inatarajia kutangaza mchezaji mwingine saa tano kamili za usiku leo kuelekea kufungwa dirisha la usajili la mwezi Januari.

Klabu ya Simba imetangaza kupitia mitandano yake ya kijamii kua saa tano kamili za usiku inatarjia kumtangaza mchezaji mwingine ambae wamemsajili katika dirisha hili la mwezi Januari. Klabu ya Simba jana iliweza kumtangaza kiungo wa kimataifa wa Burkinafaso Ismael Swadogo hivo na leo inatarajia kushusha chuma kingine.simbaWekundu wa Msimbazi kupitia mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo Salim Try Again alisema kua watafanya usajili mzuri wa kuimarisha kikosi chao kwenye dirisha dogo la mwezi Januari, Na kutokana na hali ilivyo mpaka sasa inaonesha klabu hiyo ipo kwenye mkakati wa kweli wa kuboesha kikosi chake.

Mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu Tanzania Bara kwasasa klabu hiyo inajiandaa na michuano mingine ikiwa nchini Dubai kwenye mapumziko mafupi, Lakini huku viongozi wakiendelea kuhakikisha klabu hiyo inaimarika kwelikweli.simbaKlabu ya Simba ipo kwenye mkakati maalumu wa kuisuka timu hiyo kuelekea michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, pamoja na kutaka kuurejesha ubingwa ambao wameupoteza msimu uliomalizika mbele ya watani wao klabu ya soka ya Yanga.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.