SIMBA KWAO NI FURAHA TU

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kila kitu kinakwenda sawa ndani ya timu hiyo huku furaha ikiwa kubwa kuelekea msimu wa 2023/24.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa wanatambua msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa hilo haliwafanyi wasiwe na furaha.SimbaIpo wazi kuwa Julai 12, 2023 msafara wa Simba uliweka kambi Uturuki huku baadhi ya viongozi wakibaki Bongo kukamilisha masuala mengine muhimu ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa jezi na maandalizi kuelekea Simba Day.

Ally amesema: “Maandalizi kwa ajili ya msimu mpya yanaendelea na kwetu ni furaha kuona wachezaji wanafurahia kile wanachokifanya hivyo ni muda wa kuendelea kusubiri burudani zaidi kutoka kwa Mnyama.SimbaSimba Day ni Agosti 6, 2023 na hiyo inakuja kutokana na kuwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate mbele yetu lazima wachezaji wapate muda wa kupumzika na kuwapa furaha Wanasimba,” alisema Ally.

Acha ujumbe