Simba: Baada ya Kupoteza Mchezo wao wa kwanza kwa bao 1-0 wa hatua ya Makundi ya Ligi ya mabingwa ya wanawake, dhidi ya AS FAR ambao ni wenyeji wa mashindano hayo.
Kwa mara nyingine tena Mabingwa wa kombe la CECAFA, Simba Queens watashuka dimba kutupa karata yao ya pili dhidi ya DETERMINE GIRLS kutoka Liberia.
DETERMINE ni sawa na Simba, wote walipoteza mechi zao za kwanza. Simba walifungwa na AS FAR RABAT kwa bao 1-0 na DETERMINE walichapwa 4-0 na Green Buffaloes ya Zambia.
Simba na Determine wote wanahitaji alama tatu ili kufufua matuini yao ya kufuzu nusu fainali. Mchezo huu utapigwa saa 1:00 usiku kwa saa za Tanzania.
Mchezo wa mwisho Simba watacheza NOVEMBA 5 dhidi ya Green Buffaloes. na ndipo itajulikana hatma ya Malkia hawa wa Bongo kuwa wataenda hatua inayofuata au watarejea nyumbani.