YANGA KUJIKAZA KISABUNI KWA MAMELODI

UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba hauna tatizo na wapinzani wao kwenye anga la kimataifa Mamelodi Sundowns kwa kuwa vita yao ni ndani ya dakika 90 uwanjani.

Yanga wameweka wazi kuwakama kuna mashabiki wao ambao wapo Tanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kikubwa ni kuona wanapata burudani kwenye mchezo huo wa kimataifa unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.YANGAYanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ina kibarua cha kusaka ushindi ndani ya dakika 90 kwenye hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ikisaka tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa maandalizi makubwa yanafanyika kwa timu hiyo kuelekea Machi 30 na malengo ni kupata matokeo chanya kuelekea mchezo huo ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa.

“Sisi hatuna vita na Mamelodi, hatuwachukii, kama wapo wengi waje kwa wingi uwanjani. Yanga SC lugha yetu ni amani, hatupigi wala kuzuia mtu kuja kwa Mkapa.YANGAKama mnataka kwenda kuwapokea ndugu zenu nendeni wanafika Alhamisi. Ugomvi wetu na Mamelodi utakuwa kwenye Dakika 90 Uwanjani. Wote mnakaribishwa kwa Mkapa.

“Tunatambua ni mchezo mgumu na mashabiki wanatambua umuhimu wa kupata ushindi kwenye mchezo huo hivyo wajitokeze kwa wingi kushuhudia mchezo wetu ambao ni mkubwa,”.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.