SHIRIKISHO la soka barani Afrika (CAF) wametangaza vinyang’anyiro mbalimbali kueleka tuzo za CAF 2023 maarufu kama CAF AWARDS ambapo klabu ya Yanga ipo kwenye kipengele cha kuwania tuzo ya klabu bora ya mwaka.
Yanga kutoka Tanzania inawania tuzo hiyo dhidi ya klabu nyingine tisa za Afrika ambapo hafla itafanyika Desemba 11, Marrakech nchini Morocco.Yanga ipo kwenye kinyang’anyiro pamoja na klabu za Mamelodi Sundowns na Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini. Wapo na mabingwa wa kihistoria Afrika Al Ahly ya Misri.
Klabu ya ES Tunis kutoka Tunisia, Raja Athletic Club na Wydad Athletic Club kutoka nchini Morocco. CR Belouzdad na USM Alger zote kutoka Algeria na Asec Mimosa Ivory Coast.
Yanga ndio klabu pekee kutoka Afrika Mashariki na ukanda wa Cecafa kwenye tuzo hizo.Lakini wakati huo huo golikipa Djigui Diarra wa Yanga anawania tuzo ya Golikipa Bora Afrika kwenye tuzo hizo. Diarra, anachuana na Andre Onana wa Cameroon na Man United, Edou Mendy wa Senegal na Yaccine Bounou wa Morocco.
Wengine ni Mohammed El Shanawy wa Misri, Oussama Benbot wa Algeria, Youssef El Motie wa Morocco, Pape Mamadousy wa Senegal na Landing Badji wa Senegal pia.