Kiungo wa Klabu ya Yanga, Mukoko Tonombe, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba msimu wa 2020/21.
Mwezi huo wa Oktoba, Yanga ilicheza michezo minne, ikiwa ndiyo timu iliyoshinda michezo yake yote na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom inayoshirikisha timu 18.
Mukoko amemshinda nyota wa Azam FC, Prince Dube na mshambuliaji wa Gwambina FC, Meshack Abraham aliongia nao fainali, ambapo Dube aliiongoza Azam kubaki kileleni baada ya kuvuna pointi 10 katika mwezi huo, ikishinda tatu, sare moja na kupoteza mmoja, huku mshambuliaji huyo akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za usaidizi wa mabao.
Kwa upande wa Meshack aliiongoza Gwambina kupata pointi nane ikishinda michezo miwili, sare mbili na kupoteza mmoja, ikipanda kutoka nafasi ya 17 hadi ya 14 akiifungia timu yake mabao manne.
Kaze amewashinda Aristica Cioaba wa Azam FC na Francis Baraza wa Biashara United ambapo Kaze aliiongoza Yanga katika michezo mitatu na kushinda yote.
Cioaba aliiongoza Azam kushinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza mmoja, huku Baraza akiiongoza Biashara kushinda michezo mitatu na kupoteza miwili ikipanda kutoka nafasi ya saba hadi ya nne.
Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!



Fatuma kasomo
Gud news
Sauda
Hongera yao
zeiyana
Tumeona kazi ya kanze clabuni hapo pongezi nyingi ziende kwa uwongezi wa yanga akuna mtu hasiye penda kupata tunzo kwa kweli kazi zao na juudi zao ndio zimefanya hadi kuonekana kwako naimani mengi tutayaona kutoka kwao na siku zote nyota njema huwonekana hasubui
Fatina mfingi
Pongezi kwako mukoko!!
Carolyn
Hongera zao
Adelta
Pongezi kwao club ya yanga
Angelina
Anastahili tuzo mukoko
magdalena
mukoko kaonesha juhudi kubwa sana tangu mwanzo mwa msimu
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri hongera yake
Dorophina
Pongezi kwa mukoko
Tatu
Pongezi kwa mukoko
Antony Luseno
Mukoko hivi karibuni ameonyesha kiwango kizuri sana kwa kweli anastahili
Hopemwaikuka
Gud job
Issa
Hii ndio yanga bana rekod zaid zinakuja
Povel
Congrats MUKOKO ,na KAZE🤝🤝🤝
aisha
Hongera kwao ni safi kwaklabu
Ester jackson
Hongera sana mukoko
Janeflora malisa
Hngr
David Pere
Tumeona kazi ya kanze clabuni hapo pongezi nyingi ziende kwa uwongezi wa yanga akuna mtu hasiye penda kupata tunzo kwa kweli kazi zao na juudi zao ndio zimefanya hadi kuonekana kwako naimani mengi tutayaona kutoka kwao na siku zote nyota njema huwonekana hasubui
Saupha mohamed
Pongezi sana
Sabrina
Hongera zao
Mwajumah
Pongezi kwao
Rahma
Hongera yao