Klabu ya AC Milan inatajwa kuwa tayari kuvaana uso kwa uso na Arsenal katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Manchester City, Raheem Sterling msimu huu wa joto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hajaweza kupata nafasi ya kuanza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Pep Guardiola na anaripotiwa kuwa kwenye hatua za kuondoka kuanzia msimu wa 2022-23 na kuendelea.

Sterling pia bado hajasaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Premier League baada ya msimu wa joto wa 2023, na kuiacha City katika wakati mgumu kuhusu mustakabali wake.

The Citizens wanaweza kukubali ada iliyopunguzwa kwa mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool ili kuepuka kumpoteza kwa uhamisho wa bure msimu ujao, na hatarajiwi kukosa wanunuzi.

Barcelona walitajwa kuwa kwenye mpango wa kumrudisha Sterling pale Camp Nou kwa mkopo mwezi Januari, lakini matatizo ya kifedha yanayoendelea ya Wacatalunya, yanafanya uhamisho wa majira ya kiangazi uonekane mgumu.

Sterling anamfahamu kocha wa Arsenal Mikel Arteta vyema tangu alipokuwa Luteni wa Pep Guardiola, akiwa na Calcio Mercato sasa wanadai kwamba Mhispania huyo anataka kuungana na mchezaji wake wa zamani huko Emirates.

Wakati Guardiola akionekana yupo tayari kufungua roho Raheem Sterling aondoke klabuni hapo, AC Milan wametajwa kuingia mchezoni kuisaka saini yake.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa