Akumbukwe na Aheshimiwe Johan Cruyff

Suala la ni nani anastahili kupewa heshima ya mchezaji bora wa soka wa muda wote bado limekua kitendawili kwa wengi, swali ni rahisi sana ila majibu yake tu ndio magumu. Ugumu wa kupata jawabu katika suala hilo unatokana na ukweli kwamba hilo ni suala la maoni na mapenzi binafsi ya mtu. Wakati mtu A anavutiwa na mchezaji anayefunga sana magoli, mtu B anavutiwa na yule anayepiga sana chenga! Hao watu ukiwaambia wakutajie mchezaji bora kila mtu atakupa jina la mtu anayeona anaweza kufanya kile yeye anakipenda.

Sio katika soka tu, hata katika muziki wa au michezo mingine bado suala la kupata mchezaji bora wa muda wote limekua la mjadala mkali usiofikia Mwishoni kwa miaka na miaka, imefikia hatua kila mtu ameamua abaki na anachokiamini. Huwezi kumshawishi shabiki wa Notorious Big kuwa Tupac alikua bora zaidi, mtabishana sana na pengine mkakwazana muishie kupigana.

Pamoja na ugumu uliopo katika kuamua nani ni mchezaji bora wa muda wote, ila kuna namna tu utajua tofauti kati ya mtu anaefuatilia soka na yule asiyejua chochote kuhusu huu mchezo. Chukulia mfano una watu wawili na ukawaambia wote wakutajie wacheza soka bora watatu wa muda wote kwa maoni yao, wakakutajia hawa wafuatao kwa mpangilio wowote ule. A “Maradona, Pelle, Messi” na B “Balotelli, Lingard, Pogba”! hata kama hukubaliana na A kwa namna moja au nyingine, bila shaka utachagua kumpuuza B na kuamini hana analolijua katika soka.

Nilipata bahati ya kuangalia kipindi cha luninga cha The Football Show kinachorushwa hewani na kituo cha Sky Sports, nikawashuhudia wachambuzi mahiri wa kipindi hicho yani Graeme Souness, Jamie Redknapp, Paul Merson na Alan Smith wakipata fursa ya kutaja wachezaji wao watano wa muda wote.

Wote wanne waliwataja Messi, Maradona, na Christian Ronaldo kwa mpangilio tofauti tofauti. Huku watatu, ukimtoa Paul Emerson walimtaja Pele.Emerson yeye alimalizia orodha yake kwa kuwaweka Marco Van Bastern na Paolo Maldini huku Jamie na Souness wakihitimisha na Zinedine zidane ‘Zizzou’.

Kitu kimoja muhimu kuhusu hizo orodha zao ni kwamba zinaweza kuwa au zisiwe sahihi kwa kila mtu kwa asilimia 100, lakini ni ukweli usiopingika kuwa mawazo ya wote hapo au mmoja kati yao yanarandana kwa angalau asilimia 75 na kila mpenda soka. Mimi naungana nao mkono kabisa, lakini nawalaumu kwakua wamechukua muda wangu mwingi sana, nimejikuta nikirudia kuyasikiliza hayo maoni yao zaidi ya mara mbili kuna jina nikitegemea kulisikia lakini bado sikufanikiwa kusikia. Wote hawakumtaja ‘fundi’ wa Kidachi Yohan Cruyff!

Si wao tu, mashabiki wengi wa mpira duniani ni kama huwa wanampuuzia hivi jamaa. Wanajisahaulisha kabisa kuhusu Cruyff.

Mimi huwa naona sio sawa kutaja wachezaji bora wa soka, Tena watano wa muda wote halafu ukaacha kumtaja Cruyff. Neng’eneka ujuavyo, taja Messi au Ronaldo. Ama utaje Pele au Maradona, lakini unaachaje kumtaja Cruyff?

Simtaji Yohan Cruyff eti tu kwa sababu alishinda makombe tisa ya ligi kuu ya Uholanzi maarufu kama ‘Eredivisie’ akiwa na Ajax, hapana.

Kitu kimoja muhimu kuhusu hizo orodha zao ni kwamba zinaweza kuwa au zisiwe sahihi kwa kila mtu kwa asilimia 100, lakini ni ukweli usiopingika kuwa mawazo ya wote hapo au mmoja kati yao yanarandana kwa angalau asilimia 75 na kila mpenda soka. Mimi naungana nao mkono kabisa, lakini nawalaumu kwakua wamechukua muda wangu mwingi sana, nimejikuta nikirudia kuyasikiliza hayo maoni yao zaidi ya mara mbili kuna jina nikitegemea kulisikia lakini bado sikufanikiwa kusikia. Wote hawakumtaja ‘fundi' wa Kidachi Yohan Cruyff!

Wala simuoni kuwa bora kwa sababu tu alipotua Barcelona alibeba taji la La Liga katika msimu wake wa kwanza tu na katika msimu huo huo akapewa tuzo ya mchezaji bora wa bara la Ulaya.

Na pia sio kwa sababu mwaka 1971, mimi nikiwa na umri wa miaka -22, yani miaka 22 kabla ya mimi kuzaliwa jamaa alichukua tuzo yake ya kwanza ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or kabla hajafanya hivyo tena mwaka 1973 na 1975!

Lakini pia siyo kwa sababu alifanikiwa sana akiwa mchezaji na zaidi akiwa kocha. Ikumbukwe kuwa Yohan Cruyff alikuwa kocha mwenye mafanikio sana katika vilabu vya Ajax na Barcelona ya Hispania.

Sisemi kuwa Cruyff ni mchezaji bora eti kwakua alifanikiwa kuwa kocha wa mfano kwa makocha kama Mauricio Pochettino, Sir Alex Ferguson, Arsène Wenger, Luis Enrique, Pep Guardiola, Mauricio Pochettino na wengineo wengi kwa falsafa yake maarufu ya soka ‘Total Football’.

Bali naamini kuwa Yohan Cruyff ni miongoni mwa wachezaji bora wa muda wote kwa sababu ya hayo hapo juu na mengine mengi ambayo sijaweza kuyaainisha kutokana na ufinyu wa nafasi. Hivyo ningependa kuwakumbusha kuwa, mkiwa katika vijiwe vyenu vya kahawa mkibishana kuhusu Pele na Maradona au kuhusu Ronaldo na Messi, tafadhali sana msijisahaulishe kuhusu ‘mwamba’ Yohan Cruyff.

13 Komentara

    Mholanzi fundi wa muda wote

    Jibu

    Anajua sana huyo

    Jibu

    yuko poa san

    Jibu

    amakweli cruyff ni mmoja wa magwiji wa mpira kwa wakati huo kama ilivokua kwa kina cristiano na mess kwa sasa, kwa wakati huu kuna baadhi watasema ni Ronaldo ama Mess

    Jibu

    Huyo ni jembe sana

    Jibu

    Kila nyakat zinakua na mfalme wake wa soka kama ilivyo sasa kwa mess na Ronaldo

    Jibu

    Hakuna atakaye mrithi Cruyff kwa kipi hichi

    Jibu

    He is a true Legendary.

    Jibu

    amefanya makubwa kwa kipindi chake

    Jibu

    Yuko POA sana

    Jibu

    Fundi cryuff ameacha historia kubwa pia

    Jibu

    Cryuff hongera Sana kwa kuacha historia nzuri Sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.