Alex Collado ameondoka kwenye kambi ya Barcelona ya maandalizi ya Pre-season kule Ujerumani Jumapili.
Taarifa zinasema nyota huyu ameondoka ili kwenda kuweka sawa ishu ya hatma yake na klabu ya Barcelona.
Nyota huyu alionekana akiondoka kambini pamoja na Joan Laporta na Ramon Planes. Inabainishwa kuwa staa huyu anweza kuondoka kwa mkopo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Alex Collado hajawa mmoja ya wachezaji wanaokubalika sana na Ronald Koeman, ambaye anapendelea kumtumia zaidi Yusuf Demir kuelekea msimu mpya.
Mchezaji huyu, tayari alishabainisha kuwa hana mpango wa kurejea tena Barcelona B kwa msimu mpya, akitazamia kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona au kuondoka klabuni hapo.

Vilabu kadhaa vya Hispania vinatajwa kuwa vimeulizia hali yake, na vilabu vya Bundesliga pia vikifuatilia hali yake kwa ukaribu zaidi.
Barcelona wanatajwa kuwa wapo tayari kupokea €5m. Mkataba wa sasa wa Alex Collado unaisha mwaka 2023, hivyo anaweza kuondoka kwa mkopo kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya huku akitarajia uhamisho wa kudumu kwa siku zijazo.
SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!



Issa
Ni shida