Zikiwa zimepita saa 72 toka Zinedine Zidane ajiuzuru kama kocha wa Madrid, sasa ni rasmi Madrid wamemtangaza Carlo Ancelotti kurudi katika timu hiyo na amesaini kandarasi ya kuhudumu mpaka 2024.

Ancelotti ambaye alikuwa akihudumu Everton ameng’olewa klabuni hapo na ada ya kuvunja mkataba italipwa hivi karibuni. Ancelotti alijiunga na Everton mwaka 2019 na alikuwa na msimu mzuri katika timu hiyo huku akishinda mechi saba za mwanzo kabla hali kuwa tete.

Katika taarifa iliyotolewa hivi karibuni ilieleza kuwa Carlo Ancelotti alilazimika kuondoka Everton kufuatia hofu ya kuweza kufukuzwa klabuni hapo ambayo ingeweza kumkuta kutokana na kumaliza msimu vibaya.

Carlo anarejea Madrid huku na mambo mengine yanatokea, atalipa Euro Milioni 6 kwa mwaka na kandarasi yake itadumu mpaka 2024, atamuongeza Pintus katika benchi lake la ufundi, atamuongeza mkataba Lucas Vazquez huku akianzisha mazungumzo na Ramos kuhusu kuongeza mkataba.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

6 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa