Makamu Mwenyekiti wa Yanga Arafat Haji amemsifu kocha mkuu wa klabu hiyo pamoja na benchi la ufundi kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo na kuweza kupata matokeo kwenye mazingira magumu.
Arafat: Nabi ni Fundi wa Kusoma Mchezo

Arafat alisema tangu msimu huu umeanza kwenye ligi ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika kocha Nabi na wasaidizi wake wameonyesha kitu cha utofauti kwenye mechi zote walizocheza hasa kuweza kusoma mchezo na kuweza kubadili ngumu kwa haraka na kuweza kupata ushindi.

Akizungumzia kuhusu Yanga kuendelea kufanya vizuri kwenye ligi ya mabingwa Arafat alisema: “Naamini tutasonga mbele zaidi kwa sababu timu yetu imebadilika na kuwa bora zaidi. Kocha Nabi na wasaidizi wake wamekuwa na uwezo mkubwa sana wa kusoma mchezo.

Arafat: Nabi ni Fundi wa Kusoma Mchezo

“Hilo ndiyo jambo ambalo tunalihitaji sana kwa sasa na naamini litasaidia sana kwetu kuweza kusonga mbele na kwenda mbali sana kwenye ligi ya mabingwa.”

Yanga watacheza na Al Hilal kweye mchezo wa kwanza utakaochezwa Oktoba 8 hapa Dar na kisha baadae watasafiri kwenda Sudan Oktoba 15 kucheza mechi ya marudiano. Mshindi wa jumla atakwenda hatua ya makundi.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa