Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali nchini Italia, Arsenal wamewasilisha ofa ya awali ya kumsajili Joaquín Correa.

Nyota huyu wa Lazio, mwenye miaka 26 amefunga magoli 11 kwen ye mechi 38 msimu uliopita, na mkataba wake wa sasa kluendelea kuwepo Stadio Olimpico.

Kwa mujibu wa ripoti nyingi nchini Italia, pamoja na Il Messaggero na La Repubblica, Biancocelesti wamepokea zabuni ya awali ya milioni 20 kutoka Arsenal, wakati The Gunners wakiwa wanasaka mshambuliaji msimu wa joto.

Kwa mujibu wa LaLazioSiamoNoi, Everton pia wanavutiwa na huduma ya fowadi huyo wa Argentina, lakini Lazio wanataka angalau €35m kumuuza.

Lakini, Il Messaggero wanaripoti kuwa kocha mpya wa Lazio, Maurizio Sarri aliitaka klabu kutowauza wachezaji wao muhimu kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya joto na Correa ni miongoni mwa wale ambao Sarri anataka kuwabakiza Stadio Olimpico.

Joaquín Correa, zao la akademi ya River Plate, alijiunga na Biancocelesti kutoka Sevilla kwa mkataba wa € 15m mnamo 2018. Ana mabao mawili katika mechi tano na timu ya kitaifa ya Argentina.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa