Arsenal Yahusishwa na Diamonde

Klabu ya Arsenal inahusishwa na mlinzi wa eneo la kati anayekipiga katika klabu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno raia wa kimataifa wa Ivory Coas Ousmane Diamonde.

Arsenal inahusishwa na beki huyo ambaye amekua akifanya vizuri ndani ya klabu ya Sporting Lisbon vinara wa ligi kuu nchini Ureno, Ikielezwa vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza wanataka kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ulinzi kuelekea msimu ujao.arsenalBeki Ousmane Diamonde mwenye umri wa miaka 20 tu ana uwezo mkubwa sana wa kuzuia kuanzia kushinda mipira ya nchini na juu, Lakini pia uwezo wake mkubwa wa kuweza kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma na kuipeleka timu mbele ni jambo ambalo linaelezwa limevutia maskauti wa Arsenal.

Beki Ousmane Diamonde licha ya umri wake mdogo amekua moja ya wachezaji muhimu zaidi kwenye kikosi cha kocha Ruben Amorim msimu huu akicheza beki wa kati aksihirikiana na beki wa kimataifa wa Ureno Goncalo Inacio wakitengeneza pacha bora kabisa kwenye kikosi hicho.arsenalOusmane Diamonde licha ya ubora mkubwa ambao anauonesha ndani ya Sporting Lisbon msimu huu lakini bado ana chumba cha kuendelea kuboresha uwezo wake na kua bora zaidi ya hapo, Hivo washika mitutu hao wa London wakifanikiwa kumnasa beki huyo watakua wamelamba dume kwani umri pia unambeba.

Acha ujumbe