Klabu ya Atletico Madrid inaripotiwa kuwa inavutiwa kumsajili nyota wa Manchester United, Aaron Wan-Bissaka msimu huu wa joto.

Nyota huyu wa miaka 24 amekuwa na kipindi kigumu cha msimu wa 2021-22, huku Man United wakipoteza fomu yao hivi karibuni.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, Atletico imemtambua Wan-Bissaka kama nyota anayeweza kuwa mbadala sahihi wa Sime Vrsaljiko ambaye kwa sasa anajiandaa kuondoka klabuni hapo.

Kwa mujibu wa ripoti, Bosi wa Atletico Andrea Berta tayari amekuwa akifanya mawasiliano na klabu ya Manchester United. Man United pia wanaripotiwa kuwa tayari kukamilisha dili hilo.

Bosi wa sasa, Erik ten Hag anatajwa kuwa hana mpango wa kusalia na Wan-Bissaka msimu huu wa joto na wapo tayari kumuacha mlinzi huyu aondoke kwa mkopo, pamoja na chaguo la uhamisho wa kudumu.

Wan-Bissala pia amekuwa akihusishwa na klabu ya Roma chini ya Meneja Jose Mourinho na pia klabu yake ya zamani ya Crystal Palace. Mkataba wake wa sasa na Man United unafika tamati Juni 2024.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa