Nyota wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic ameweka wazi kuwa hana uhakika juiu ya Hatma yake Milan. Staa huyu pia amesisitiza kuwa bado hajafahamu ni nini anachokihitaji kwa sasa.
Zlatan amesema mambo yamekuwa yakibadilika kwa kasi kila siku kiasi kwama sio rahisi kufahamu nini kitatokea. Alirejea kutoka MLS mwezi Januari alipokuwa LA Galaxy na kutoa mchango mkubwa klabuni hao kwenye michuano ya Coppa Italia na Serie A.
Staa huyu amefunga magoli 4 katika mechi 10 za Serie A na Coppa Italia, mkataba wake unaisha mwezi Juni na inaripotiwa kuwa staa huyu mwenye miaka 38 hataweza kuongeza mkataba.
Kwa upande wake anasema bado hajajua nini anataka
“Tutaona, Sijajua nini nataka bado, Kitu kipya kinaonekana kutokea kila siku. Italia ni nyumbani kwangu kwa pili na ilikuwa safi kucheza tena San Siro.”
-Zlatan Ibrahimovic
Staa huyu anasema kwa sasa hatakiwi kuendelea kufikiria kuhusu yeye tuu, anahitaji kufurahia maisha yake na wapendwa wake kwa kuwa ana familia ya kuiangalia. Maneno ya Ibra yanaashiria kama hatarajii kusalia Milan baada ya kumaliza mkataba wake.


Hope mwaikuka
Hata hvyo umri umeenda tulia tu
Issa
Zlatan jembe tu