Barcelona Kutia Mguu kwa Matthijs De Ligt!

Barcelona wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi kwa kumsajili Matthijs de Ligt kutoka Juventus, kwa mujibu wa ripoti ya Diario Sport.

Kipaumbele cha Blaugrana kwa soko lililobaki la usajili la Januari ni kusonga mbele na kupunguza bili yao ya mishahara, lakini tayari wanatazamia ununuzi wa msimu wa joto.

Inasemekana Xavi anavutiwa na De Ligt, ambaye alijiunga na Juventus kutoka Ajax msimu ambao Barcelona ilimsajili swahiba wake Frenkie de Jong.

Kifungu cha kuachiwa kwa De Ligt huko Turin ni euro milioni 125, na inaeleweka kuwa Juventus wanataka kurudisha euro milioni 80 walizoilipa Ajax.

Kuna imani pia kwamba Mino Raiola, wakala wa De Ligt, ameiambia Barcelona kwamba ana kifungu cha kuondoka kilichojadiliwa na Juventus haswa kwa ajili yao ambacho ni chini ya € 125m.

De Ligt mwenye miaka 22, ametumia maisha yake yote akiwa na Ajax kabla ya kwenda Serie A. Ameichezea timu ya taifa ya Uholanzi mara 33.


KUWA MILIONEA MSIMU WA SIKUKUU NA SAHARA RICHIES

Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.