Mshambualiaji wa zamani wa Brazil Giovance Elba anasema kuwa Barcelona hawatakiwi kumsajili tena nyota wao wa zamani Neymar, ambaye aliamua kuhamia Ufaransa.
Neymar ambaye kwa sasa ana miaka 28, amekuwa akihusishwa mara kwa mara na duru za soka kuwa anatarajiwa kurejea klabu ya Barcelona. Ni kama ana miaka mitatu tangia atoke Barcelona kwa ada ya kuvunja rekodi ya dunia ya paundi milioni 222.
Elber ambaye aliwahi kung’ara sana wakati akiwa Bayern Munich, ambaye alicheza gemu 15 za timu ya taifa ya Brazili katika maisha yake ya soka, anaona kama mabingwa wa La Liga, Barca wangeacha kabisa kufikiria kumrejesha Neymar new Camp na anahoji kuwa ‘hawajiulizi kwa nini aliamua kuondoka klabuni hapo?’
Akiwa kwenye mahojiano na Cadena SER aliulizwa Barcelona wamsajili Neymar tena? Elber akajibu “Hapana. Kwa kuwa aliondoka Barcelona kwangu hakuna uwezekano wa kurejea hapo tena”
Elber anasea Neymar aliondoka bila heshima alipokuwa anaondoka Barca, kwa kuwa aliondoka kwa kusema kuwa anataka kwenda kuwa bora zaidi duniani akiwa PSG.
Kama Elber, angekuwa ni sehemu ya maamuzi muhimu Barcelona basi Neymar asingekuwa na nafasi9 tena Barcelona.


lombo
neymar anajua ila ubshooo unamwalibia
sylvester
Neymar anafuata soko la sasa la pesa tunaita mpira pesa sio kama kipindi cha Elber mm nafkiri Barcelona kumrudisha Neymar ni jambo zuri sana
Gabriel
Good news 👍# meridianbettz
Adelta
nkwel cz ameshachuja
Dorophina
Neymar anajua sana kucheza mpira na mpira wake ni wa kiwango
Tahiya
Elbar haache wivu mana mchezaji kuhama timu na kurejea ni jambo la kawaida
Lydia Emmanuel Magoti
Neymer anajua yupo vizuri kisoka ila ubishoo mwingi ndomana anashuka kimpa Sasa Kama analudi Barcelona nivizuri
Amani
Barcelona kumrudisha Neymar ni jambo zuri sana#meridianbettz
Salma
Wacha wivu
Samiah
Neymer anajua ila analewa sana sifa
Hope mwaikuka
Ila iko kijamaa nacho kinajiona sana ndo maana anapotea
Khadija
Barcelona kumrudisha Neymar no Mambo zr#meridianbettz
Furahav
Wamuache kwan hana majabu tena.
Khadija
Barcelona kumrudisha Neymr ni jambo zuri
Hope mwaikuka
Bora wamchukue huko kafulia na aache ubishoo
Emmy cleopa
Bora barcelona wamludishe neymar huyo ni fundi.
#meridianbettz
Povel
Thanks meridian kwa gud news za Kimichezo na burudani
Neema hassan
Neymar kurudi barcelona jambo la busara#asante meridianbet kwa taarifa..
Agness
Neymar yupo vizuri is namba one
aisha
Ahsanteni meridianbet kwa taarifa
frank patrick
Atakuwa na kazi kubwa kwa mashabiki wa Barca itambidi auvae uCristiano Ronaldo
Theckla
Barcelona wamrudishe tu yuko vizuri
Mwanahamisi
Asante meridian kwa taarifa
Ester mmakasa
Basi akae hapo alipo sasa coz aliondoka mwenyewe.
Furahav
Hana jipya.
Mwajuma
Neyma Yuko vizuri anastahili
SADICK
Nakubaliana nae kwa 100%. Hakuna sababu ya kumurejesha Neymar Barcelona#meridianbettz
felister
Hana haja kurudi tena barcelona
Rehema Dickson
Yuko vizuri ila ana madoido sana
Antony Luseno
Naungana na Elber kiwango cha Neymar kimeshuka
Mwanaidi
Duuh mambo hayo
Rehema
Ni fundi sn ila ni Bishop sn uwanjan
Ernest
Elber kaongea vizuri tena kifundi lakini mpira wa sasa unaangalia sana umuhimu wa mchezaji flani kuwepo ndani ya kikosi, kwa Barca Neymar bado ananafasi na kama ataendelea kukaza Buti basi Mikoba ya Messi itamfuata kwani Messi umri unamtupa mkono, Namaanisha Ufalme ndani ya Nou Camp.
Mwajuma
Meridianbettz mpo vizur kwa habari za michezo
Carolyne
Neymar yupo vzr
mwakalosi
Huyu keshakuwa sharobaro sio tena mchezaji hatari
Warda
Elba ana wivu tu
Isaya massawe
Neymar ubishoo mwingi
Ester jackson
Elber aache wivu alitaka kumpelekesha neymar kisa anajua aache arudi tu hayo yashapita
Zeiyana iddi
Neymar alikua hanataka kua staa za ya pale..!kaona kucheza mpira na messi hatakua haonekane ndio maana hakaamua hajitenge..!sio mbaya kila mtu na maamuzi yake msameeni tu mambo yaendelee..!!
Evaluziga
Anajua Sana Ila bishoo
uwanjani
David pere
Neymar waachane naye bado Ana utoto sana
Juliana
Neymar anamaajabu tena, kama vip wasimsajili tu
Neema juma
Hiyo ni Roho mbaya aisee. Eto ‘o ni mchezajii mzuri mno.
Genia skaluzwe
Ubishoo mwingi Sana huyo Mpira hakuna hapo
farida ahmadi
Neymar ni mchezaji mzuri Sana