Barcelona waweka rekodi tena

Klabu ya Barcelona imefanikiwa kuandika rekodi tena baada ya timu ya taifa ya wanawake ya Hispania kutwaa kombe la dunia leo nchini Australia baada ya kuifunga Uingereza bao moja kwa bila.

Barcelona ilifanikiwa kua na wachezaji saba wanaoanza kikosi cha kwanza kwenye timu ya taifa ya Hispania ya wanaume iliyotwaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika ya Kusini, Huku leo ikijirudia tena baada ya klabu hiyo kutwaa wachezaji saba wa kikosi cha kwanza kwa timu ya wanawake wa nchi hiyo kilichotwaa kombe la dunia.barcelonaKlabu hiyo yenye maskani yake kwenye kitongoji cha Catalunya nchini Hispania ilifanikiwa kutawala soka la dunia ngazi ya klabu na ndio sababu kubwa ya kufanya vizuri na timu yake ya taifa.

Barca kwasasa timu ya wanawake ya klabu hiyo inafanya vizuri sana kama ambavyo timu ya wanaume ilikua ikifanya vizuri miaka kadhaa nyuma, Hivo wachezaji wake wengi ni raia wa kimataifa wa Hispania na ndio wanaanza timu ya taifa ya nchi hiyo.barcelonaKlabu ya Barcelona wanajivunia kufanikiwa kuweka rekodi hii lakini mahasimu zao pia klabu ya Real Madrid walikua na idadi nzuri ya wachezaji kwenye kikosi cha Hispania kilichotwa kombe la dunia leo.

Acha ujumbe