Klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania imeambuliwa kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya klabu ya Interzionale Milan katika dimba la Sansiro.

barcelonaBarcelona iliyopo chini ya gwiji wa zamani wa klabu hiyo Xavi Hernandez wamepata kipigo cha pili mfululizo katika ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kufungwa wiki kadhaa nyuma na klabu ya Fc Bayern Munich na kusalia na alama tatu katika michezo mitatu waliyocheza sasa katika kundi C.

Katika mchezo huo ambao klabu ya Barcelona walionekana kutawala kwa kiwango kikubwa sana kwa maana ya kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi lakini klabu ya Inter Milan ilionekana kucheza kwa nidhamu na kuweza kupata bao kupitia kwa Mturuki Hakan Calhanoglu na kuwafanya kupata alama tatu muhimu huku wakifanikiwa kufikisha alama sita wakishika nafasi ya pili kwenye kundi nyuma ya Bayern Munich.

barcelonaBarcelona wanahitaji kujiboresha na kushinda michezo inayofuata ili kuepuka aibu iliyowakumba msimu uliomalizika baada ya kushindwa kufuzu hatua ya 16 bora na kuangukia katika michuano ya Europe League.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa