Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp bado ameendelea kumtetea mshambuliaji wake Darwin Nunez ambae anaonekana kua na ukame wa mabao klabuni hapo.

jurgen kloppKocha huyo anaamini mshambuliaji huyo atafanya vizuri na kufunga haswa katika uwanja wa nyumbani wa klabu ni suala la muda kwa Nunez kuanza vizuri na kuanza kufunga Anfield alieleza klopp hii ni baada ya straika huyo kushindwa kufunga katika mchezo wa jana dhidi ya Rangers.

Golikipa wa Rangers Alan Mccregor aliokoa mashuti nane na Nunez alikua mchezaji wa Liverpool aliepiga mashuti mengi golini na hii inamfanya kocha wake kuamini ataanza kufanya vizuri siku za karibuni.

“Nadhani unaweza kuliona hilo. Nadhani unaona vijana walivyosonga mbele, ilikua siku nzuri kwa kipindi kimoja cha mazoezi” Tulikua na kipindi kimoja tu, Tulicheza kwa kiwango cha chini kwasababu tumecheza hivi karibuni kwahiyo ilionesha namna alivyokua mshambuliaji mzuri, akiingia kwenye hali kama hizi, Hii itatokea” Alisema Jurgen Klopp akionesha imani yake kwa mshambuliaji huyo.

jurgen kloppMshambuliaji huyo aliesajiliwa kwa gharama kubwa kutoka klabu ya Benfica ya nchini Ureno bado hajafanikiwa kuonesha makali ambayo wanazi wa klabu hiyo na wadau wa soka walitarajia lakini mwalimu wa klabu hiyo anaamini ni suala la muda mshambuliaji kuanza kufanya vizuri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa