Lionel Messi atarejea Barcelona majira ya joto mwaka 2023, baada ya kufanya ‘amani’ na rais wa klabu hiyo kufuatia kuhama kwake miaka miwili iliyopita.
Mshindi huyo mara saba wa Ballon d’Or alijiunga na PSG baada ya Barca kutoa taarifa kwamba ataondoka kutokana na vikwazo vya kifedha vilivyowekwa na LaLiga.
Hata hivyo, Messi – ambaye alijiunga na PSG mwaka wa 2021, ataripotiwa kurejea Barcelona wakati mkataba wake katika mji mkuu wa Ufaransa utakapokamilika msimu ujao wa joto.
Kwa mujibu wa taarifa nchini Argentina zilitanabaisha, Messi atarejea Barcelona Julai 1, 2023 baada ya miaka miwili pekee huko Paris Saint-Germain.
Inaaminika Messi atarejea katika klabu hiyo baada ya ‘kuelewana’ na Rais wa Barcelona Joan Laporta ambaye alikuwa katikati ya mabishano hayo miaka miwili iliyopita.
Lionelalikua mchezaji huru mnamo 2021 baada ya mkataba wake na Barca kumalizika. Hata hivyo, alitarajiwa kusaini tena klabu hiyo kufuatia mazungumzo chanya ya awali kati ya pande zote. Hata hivyo, Barca waliangusha taarifa iliyothibitisha kwamba Messi ataondoka kutokana na vikwazo vya kiuchumi na kimuundo (kanuni za LaLiga ya Uhispania).
Taarifa hiyo ilisema: “Licha ya kufikia makubaliano kati ya FC Barcelona na Leo Messi na kwa nia ya wazi ya pande zote mbili kusaini mkataba mpya leo, hauwezi kurasimishwa kutokana na vikwazo vya kiuchumi na kimuundo (Kanuni za LaLiga ya Uhispania).
“Kutokana na hali hii, Lionel hataendelea kuhusishwa na FC Barcelona. Pande zote mbili zinajuta kwamba matakwa ya mchezaji na Klabu hayawezi kutimizwa hatimaye.
“Barca ingependa kushukuru kwa moyo wake wote mchango wa mchezaji huyo katika kuimarisha taasisi na inamtakia kila la kheri katika maisha yake binafsi na kitaaluma.’
Lionel alisemekana kushtushwa na tangazo hilo kwani alikubali kukatwa asilimia 50 ya malipo kwenye mkataba wake wa awali, ambao ulikuwa na thamani ya zaidi ya paunsi milioni 425 kwa miaka minne ili kusalia klabuni hapo.
Hata hivyo, Lionel bado ana nia ya kurejea Barcelona msimu ujao – kulingana na ripoti. Lionel na familia yake wamekuwa wakiipenda Barcelona na walizungumza kuhusu kurudi siku moja.
Nyota huyo alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya wakubwa ya Barcelona mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 16 tu na alicheza mara 778, akiibuka mchezaji muhimu. Aliendelea kuwa mfungaji bora wa Barca akiwa na mabao 672 yakiwemo mabao 120 ya Ligi ya Mabingwa na rekodi ya mabao 474 ya LaLiga.