Mchezaji wa zamani wa klabu za Arsena na Barcelona Cesc Fabregas amebadili mawazo yake kwenye kinyanganyiro cha mshindi wa Ballon d’Or mwaka huu na kusema kuwa mshindi mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karimu Benzema anastahili tuzo hiyo.
Cesc Fabregas alichapisha kwenye mtandao wa Tweeter kabla ya mchezo kuanza akisema ‘mimi sio mshabiki wa tuzo binafsi lakini na hakika mshindi wa Ballon d’Or anaweza kuamuliwa usiku wa leo, Mane? Salah? Benzema?’
Mchezaji bora wa mechi hiyo golikipa Courtois ubora wake ulimfanya Cesc Fabregas abadilishe mawazo ya na kumuongeza kwenye kinyanganyiri cha moja ya wachezaji wanaoweza kushinda tuzo ya Ballon d’Or.
Cesc Fabregas alliweza kurirudia chapisho lake la tweeter na kuandika, “ningemuongeza na hakikia nitampa tuzo ya Ballon d’Or Courtois. Amekuwa na msimu bora sana.”
Wakati Fabregas akimpa tuzo hiyo mlinda mlango wa klabu ya Real Madrid, mchezaji mwingine wa zamani wa arsena Thierry Henry amepingana nae na kumpa Benzema.
Thierry Henry akizungumza na kituo acha runinga cha CBS Sports alisema, “nilikuwa nataka kusema kitu kwa waandishi au chama cha soka cha Ufaransa au yoyote anaehusika na kupiga kwenye Ballon d’Or, kula zimefungwa na mshindi ni Benzema. Kwaherini.”
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!