Benzema Atema Nyongo

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Karim Benzema ametema nyongo baada ya kuulizwa juu ya ukame wake wa mabao toka mwezi Disemba mwaka jana.

Mshambuliaji Karim Benzema amekua hana wakati mzuri sana ndani ya klabu yake ya Al Ittihad anayoitumikia kwasasa, Akisema kinachofanya asifanye vizuri ndani ya klabu hiyo ni kwakua mambo yamebadilika.benzema“Mimi sio Benzema wa Real Madrid kwasababu sio aina moja ya mchezo na sio mchezaji yuleyule, Nahitaji msaada kiwanjani nahitaji mambo mengi, Siwezi kushinda mchezo peke yanga” Alisema mshambuliaji huyo.

Kupitia mahojiano hayo mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid ameonesha anahitaji msaada kutoka kwa wachezaji wenzake ndani ya timu hiyo ili kuweza kufanya vizuri kama ambavyo alikua anafanya ndani ya miamba ya soka nchini Hispania.

Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon Dor mwaka 2022 amekua hana wakati mzuri sana ndani ya kikosi cha Al Ittihad, Jambo ambalo limefanya kuibuka kwa tetesi kua anaweza kutimka ndani ya klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia.benzemaStaa Karim Benzema alipoulizwa kuhusu kutimka ndani ya klabu ya Al Ittihad alieleza kwamba hajajua mustakabali wake, Lakini kwasasa akili yake ipo ndani ya klabu hiyo kwani habari mpya zainaibuka kila siku.

Acha ujumbe