Nyota wa Manchester United Bruno fernandes aomba radhi kwa kukosa penati dakika za majeruhi katika mchezo wa ligi juu ya uingeraza ambapo Manchester ilipoteza kwa 1-0 dhidi ya Aston Villa.
Aston Villa walipata goli la kwa kupitia Kortney Hause akionganisha kona safi iliyopigwa na Douglas Luiz dakika ya 88.

Bruno amekosa penati ya pili kati 23 alizopiga akiwa na United katika mashindano yote na ya kwanza tokea oktoba 2020 dhidi ya Newcastle kwenye mchezo wa ligi kuu.
“Hakuna aliyechanganyika na kujihisi mkosaji kuliko mimi kwa kukosa penati,kukoselewa na kutofautiana kimtazamo ni sehemu kubwa ya mpira, nimejifunza kuishi nayo.
“Leo kwa mara nyingine nilichukua jukumu ambalo nilipewa tokea nimejiunga na United, na nitalichukua tena pasipo uoga wala hofu muda wowote nitakaohitajika.
“Asanteni wote kwa ushirikiano wenu mwanzo wa mchezo hadi kipenga cha mwisho, nilisikia mkilitaja jina langu uwanjani mlinitia moyo sana, kitu muhimu kwangu ni kushinda pamoja na nitafanya chochote kuwasidia wezangu na klabu kuwa bora zaidi.” alisema Bruno
Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.



Sania+mapua
Pole sana Bruno