Kiungo nyota wa timu ya Manchester United Bruno Fernandes ambaye alipata ajari ya gari leo asubui amefanikiwa kufanya mazoezi na timu kwa pamoja kwenyemazoezi ya jioni siku ya leo.

Hakuna upande ulioripotiwa kupata majera makubwa kwenye ajari hiyo, huku Bruno Fernandes akifanikiwa kufanya mazoezi na timu ambayo inajiandaa kwenye mchezo wake wa Jumanne dhidi ya Liverpool kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Bruno Fernandes

Kocha wa muda wa klabu ya Manchester United amethibitisha kuwa Fernandes atakuwepo kwenye kikosi kitachowakabili Liverpool licha kupata ajari leo.

‘Ndio amefanya mazoezi na timu,” alisema. “Bila shaka, ajari ilitokea wakati akiwa njiani kuja mazoezini, lakini hadi sasa ninavyofahamu, hakuna aliyeumia.

“Bruno Fernandes alikuwa mazoezini na timu na alikuwa sawa tu, ndio maana nadhani atakuwa sawa kwenye mchezo wa kesho.”

Bruno Fernandes mpaka amefanikiwa kuifungia klabu hiyo magoli tisa na kusaidia kupatikana magoli sita kwenye michezo 30 ya ligi kuu kwenye msimu huu mpaka sasa.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa