Klabu ya Chelsea mpaka sasa bado wako kwenye vita ya kimaslahi kati ya Romelu Lukaku na klabu ya Inter Milan huku kila mmoja akivutia kwake kuhusu uhamisho huo.

Chelsea wanahitaji kumuuza au kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake Lukaku, lakini hawako tayari kumtoa bure na wametoa ada yake ya uhamisho ambayo ni €10milioni, huku klabu ambayo imeonesha nia, yakuhitaji  huduma ya mchezaji huyo na mchezaji mwenyewe angependa kwenda kuitumikia ni klabu ya Inter Milan.

Chelsea

Inter Milan wanahitaji hudumua ya mchezaji huyo lakini hawako tayari kutoa kiasi cha  €10milioni, wako tayari kulipa kiasi €5milioni kwa mwaka mmoja ambao wanahitaji kumtumia.

Awali klabu ya Chelsea, iliweka kiasi cha €24milioni kama ada ya mkopo kwa klabu ambayo itahitaji huduma ya mshambuliaji huyo, kabla ya kuishusha na kufikia €10milioni. Lukaku yuko tayari kupunguza nusu ya mshahara wake ili arejee nchini Italia kwenye klabu ya Inter Milan ili kufanikisha uhamisho huo.

Chelsea walimnunua Lukaku majira ya kiangazi yaliopita kwa kitita cha €113milioni lakini hakufanikiwa kuonyesha makali aliyokuwa nayo pindi anaitumikia klabu ya Inter Milan. Pia kuna tetesi kuwa mazungumzo bado yanaendelea ambapo Chelsea hawataki kupata hasara kwa msimu 2022-23.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa