Ni hali ya kawaida kwenye maisha kuna kupanda na kushuka. Anachokipitia Christian Eriksen ndani ya Inter Milan ni maana halisi ya kushuka kwenye maisha.
Eriksen wa Tottenham sio huyu wa Inter chini ya Antonio Konte. Kutoka kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza na kuwa mchezaji anayesugua benchi.
Japo maisha ndani ya Serie A yamemuendea kombo, Christian Eriksen bado anaikingia kifua EPL na hana mpango wa kurejea kwenye ligi hiyo.

Arsenal wanatajwa kuisaka saini ya Eriksen kwenye usajili wa dirisha dogo mwezi ujao. Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na gazeti ya Star, nyota huyu wa Denmark hana mpango wa kwenda Emirates na badala yake PSG ndio timu ambayo anaweza kujiunga nayo.
Kabla hajatimkia Inter, Man United waliihitaji saini yake kwa muda mrefu bila mafanikio na mwisho wa siku aliamua kwenda Inter lengo lake likiwa ni kubadilisha upepo na kucheza kwenye ligi nyingine tofauti na EPL.

Kama lengo lilikuwa kubadili ligi, basi kurudi EPL sio chaguo sahihi kwake hasa wakati huu ambao anaonekana mwenye kiwango duni tofauti na alivyokuwa miaka ya nyuma.
Bado ni hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya Eriksen kwenye ulimwengu wa soka. Antonio Conte anaendelea kumuweka benchi huku akimpatia nafasi Nicolo Barella. Tangu amejiunga na Inter mwezi Januari, Eriksen ameanzishwa kwenye kikosi cha kwanza mara 4 tu!
PSG wataokoa maisha ya Eriksen kutoka Serie A au ataendelea kusota chini ya Antonio Conte? Majibu tutayapa kwenye dirisha la usajili mwezi Januari 2021.
BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!



Caroline
Safi sanaaa
Rahma
Saf
Sarah
Vizuri
Dorophina
Nice update
lombo
vzr
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri
Issa
Erikseen ni noma
Hopemwaikuka
Fresh
Ernest
Kuna uwezekano mkubwa sana wa Eriksen kutua Arsenal
Mwanahamisi
Vizuri
Janeflora malisa
Safi
Saupha mohamed
Safi
samiah
Gud
Tatu
Safi
warda
imekaa vizuri