Kiungo wa zamani wa klabu ya Liverpool, Barcelona, na Bayern Munich Philippe Coutinho amefanikiwa kujiunga na klabu ya Vasco da Gama ya nchini Brazil kwa mkopo akitokea klabu ya Aston Villa.
Coutinho amefanikiwa kujiunga na klabu yake ya utotoni ambayo ilimlea kabla ya kwenda barani ulaya ambapo anajiunga na klabu hiyo baada ya kutumikia vilabu mbalimbali barani ulaya, Mchezaji huyo anajiunga kwa mkopo kutoka Vasco da Gama kutokea Villa ingawa msimu uliopita alicheza kwa mkopo pia klabu ya Al- Duhail ya nchini Qatar.“Ni hisia za furaha kubwa. Niliishi nje kwa muda mrefu, kwa hiyo ni kweli hisia za kurudi nyumbani, mahali nilipokulia, mahali ninapopapenda, klabu ninayoipenda.” Staa huyo amekua hana wakati mzuri sana tangu aondoke ndani ya Liverpool na mara nyingi amekua akitolewa kwa mkopo kwa vilabu kadhaa.
Mpaka sasa Coutinho ameshacheza vilabu vinne kwa mkopo tangu ajiunge na klabu ya Barcelona ambapo alitolewa kwa mkopo Bayern Munich, Aston Villa kabla ya baada ya kuja kununuliwa kwa uhamisho wa kudumu, Al-Duhail na sasa ametolewa kwa mkopo klabu ya Vasco da Gama.Kiungo huyo ameonesha ana furaha ya kurejea klabu yake ya nyumbani ambayo ilimkuza kisoka na inawezekana inaweza kua nafasi ya pili ya kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil kuweza kufufua makali yake ambayo aliyaonesha kwenye klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza.