De Gea Dili lake na Genoa Limekufa

Golikipa wa zamani wa klabu ya Manchester United David De Gea dili lake limeshindikana yeye kujiunga na klabu ya Genoa ya nchini Italia kutokana na mshahara.

De Gea amekua nje ya uwanja kwa mwaka mmoja sasa bila kua na timu ambayo anaitumikia na msimu huu klabu ya Genoa ya nchini Italia ilihitaji kupata huduma ya golikipa huyo, Lakini klabu hiyo imeshindwa kua na msuli wa fedha ambapo wameshindwa kumpata golikipa huyo kutokana na kushindwa kufikia mshahara wake.de geaKlabu zingine zinaelezwa kuendelea kuifatilia saini ya golikipa huyo wa kimataifa wa Hispania kwajili kumpata kwajili ya kuhakikisha anajiunga kwenye timu zao kutokana na ubora wa golikipa huyo, Lakini timu nyingi zinafeli kumalizana na golikipa huyo kutokana na mahitaji ya kimaslahi ya golikipa huyo.

Ikumbukwe kua golikipa De Gea wakati anaondoka ndani ya Man United alikua ndio mchezaji ambaye alikupa analipwa ghali zaidi, Hivo hii inakupa picha kua ni kwanini vilabu kadhaa vinashindwa kumpata golikipa huyo haswa vilabu vya daraja la kati lakini vilabu vya Saudia Arabia navyo vinahusishwa na golikipa huyo na vilabu hivo ndio vinaelezwa kua na msuli wa pesa kwelikweli.

Acha ujumbe